.

.

Chidi Benz alivyo fafanua kauli yake ya kusema hakuna rapa wa Bongo aliyefikia mafanikio yake

Rapa Rashid ‘Chidi Benz’ Makwilo, amefunguka na kusema kuwa alikuwa akimaanisha kauli yake kuwa kuna marapa Bongo ambao wametengenezwa. “Mimi kusema kuna marapa wametengenezwa sio kosa, tuseme ukweli mimi unanifananisha na nani?, tuachane na mambo niliyopitia sijui nini tuseme tu mimi unanifananisha na nani katika kuchana?, “ Alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times Fm jumamosi iliyopita.
Mkali huyo anayetamba na wimbo wake ‘Chuma’, ameeleza kuwa anawaheshimu marapa waliomtangulia kwenye ‘Game’ lakini hakuna aliyefikia alichofanya kwenye ulimwengu wa Hip Hop Tanzania. “Unaongelea kuchana au unaongelea maisha? Ya kwenye maisha tupo tofauti kuna marapa wengine hawajawahi vuta Sigar au kunywa Pombe, lakini unaongelea kuchana, Mimi mwenye tuzo tano ambazo hakuna rapa mwenye nazo Bongo, hakuna anayechana anazo mi ninazo 5, mwenye nazo ana 1 ama mbili. “Unataka kuniambia kuna rapa kafanya kolabo kama mimi?, kuna mtu karekodi kolabo zangu zimefika 392, nilishafanya kolabo na aina kibao za wasanii, muite rapa wako msimamishe hapa muulize unasemaje kuchana kati yakow ewe na Mjomba, kweli wametengenezwa” Alisema.

No comments

Powered by Blogger.