.

.

‘The little boy is a public property’ asema Huddah, aingia kwenye beef na Zari, kisa Diamond

Kila kukicha, drama mpya inazaliwa na Diamond anakuwa centre ya ubuyu.
Staa huyo alifanikiwa kuizima skendo ya kumsaliti mpenzi wake Zari kwa kudaiwa kutembea na Hamisa Mobetto kwa kuachia hit yake ‘Kidogo’ na P-Square, lakini jingine limeibuka tena wiki hii.
La sasa hivi limhusu Zari na staa wa Kenya mwenye skendo chungu mzima, Huddah Monroe na kila mtu anajiuliza limeanzia wapi!

Ni kwasababu mastaa hawa walikuwa marafiki siku za nyuma. Let’s guess tatizo limeanza baada ya kudaiwa kuwa Zari amemkaushia Huddah kumpa mwaliko kwenye birthday party ya mtoto wake, Tiffah itakayofanyika mwezi ujao.
Ikumbukwe kuwa, June mwaka huu Huddah alipost Instagram kuelezea jinsi alivyo na hamu na birthday ya binti huyo maarufu.
“Our baby @princess_tiffah Turning ONE soon…. The ROYAL DUTCHESS of TZEE . Hii Sio party ya kikosa Jamani . There will be a BIG SURPRISE that day! Asiye na wake aeleke jiwe….Mimi I’ll be there na mawe zangu khaa! Mama Tiffa @zarithebosslady give us LOCATION Basi …. We need to book tickets EARLY,” aliandika Huddah.
Lakini katika badiliko kubwa la tukio, ni hasimu wake na Huddah, Vera Sidika ndiye anadaiwa kualikwa.
“Finally, Countdown to Tiffah’s Birthday. I’m so excited kuja vile mnajua itakuwa mambo moto, Kama vile White Party,” ameandika Vera kwenye Instagram.
“As u know your parents @zarithebosslady @diamondplatnumz hawakosei wakifanya kitu. Wacha nichukue hii nafasi kusema HAPPY BIRTHDAY @princess_tiffah wangu Mungu akutunze na kukupa afya njema na ukue vyema aunty Vera anakupenda sana na amekununulia zawadi najua utayafurahia,” ameongeza.
“Kama na wewe utakuwa mmoja wapo kwa walioalikwa basi itakuwa bomba sana maana patakuwa apatoshiiii yani na Kama ujaalikwa ni tatizo maana kule ni shidaaaaaa😆. Watu na aunty Zao. Wacha niishie hapa Tukutane huko.”
Japo kunaweza kuwa na sababu nyingine kubwa zaidi nyuma ya mtifuano huo, lakini Huddah ameonekana kumind na amemrushia Zari makombora mfululizo kwenye Snapchat.
Kwa mujibu wa bidada huyo, Diamond ni mali ya umma inayoweza kugawiwa na mtu yeyote kama pizza. Kwenye ujumbe mwingine ameeleza kuwa amewahi kula chakula na wote wawili akiwaenjoy tu.
“When you think your man is yours kumbe he is ours. And I ate and dined w both of u,” ameandika Huddah.
“LOL. Having kids with someone to tie him down doesn’t mean he won’t leave,” ameandika kwenye snap nyingine.


No comments

Powered by Blogger.