.

.

Davido hajasaini na label nyingine baada ya Sony Music – ni kwa mujibu wa Uongozi wake

Hivi karibuni kuliripotiwa kuwa staa wa Nigeria, Davido alisaini mkataba mwingine na label ya RCA ya Marekani.
Na sasa uongozi wake umetoa ufafanuzi na kudai kuwa staa huyo hajasaini mkataba mpya bali RCA ni tawi la kampuni ya Sony iliyomsaini awali. 
Uongozi huo umedai kuwa kazi za Davido nchini Marekani zitasambazwa na RCA ambayo ipo ndani ya Sony.
Tayari Davido amesharekodi collabo na msanii wa Marekani, Tinashe na huenda video yake imeshakalika. Alipost picha hiyo chini ya mrembo huyo mwenye asili ya Zimbabwe kwenye Instagram.
 Tangu asaini na Sony bado staa huyo hajaachia wimbo wowote.

No comments

Powered by Blogger.